Na mwandishi wetu
Nyota wa zamani wa Simba SC, Shiza Kichuya ‘amemng’ata’ sikio winga mpya wa timu hiyo, Ladack Chasambi (pichani) kuwa kama anataka kufika mbali basi anapaswa kuwasikiliza nyota wazoefu aliowakuta hapo, watamfundisha vingi.
Kichuya alisema kuwa kinda huyo ameingia Simba ameikuta timu ikiwa imekamilika hivyo anatakiwa kupambana kwani tofauti na yeye wakati anatua mitaa ya Msimbazi walikuwa wanajitafuta.
“Simba iko tayari, sio kama ile waliyokuwa wanaunga-unga, Ladack ni mchezaji mzuri atulize akili ajue nini anatakiwa kufanya na Wanasimba wanahitaji nini kutoka kwake atafika anapotakiwa kufika.
“Lakini asiweke presha kubwa maana bado ni kijana mdogo, ameenda kwenye timu kubwa, umri wake na alipoenda ni vitu viwili tofauti, anatakiwa kupambana zaidi ya alipotoka,” alisema Kichuya.
Kichuya anayekipiga JKT Tanzania kwa sasa alimsihi Chasambi asijipe ukubwa kwani anapaswa ajue yeye bado mdogo anatakiwa kujifunza, afanye kazi kwani miongoni mwa vijana ambao mkoa wa Morogoro wanajivunia nao ni yeye na wanaamini kwa kipaji alichonacho ataisaidia Simba.
Soka Kichuya ampa neno Chasambi
Kichuya ampa neno Chasambi
Read also