London, England
Kocha wa Man City, Mauricio Pochettino amepuuza habari kuwa Chelsea inahitaji kusajili straika katika kipindi cha usajili cha Januari na amekanusha kuiwania saini ya straika wa Brighton, Evan Ferguson.
Chelsea imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika eneo la ufungaji msimu huu na katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya Fulham waliyotoka na ushindi wa bao 1-0 kwa mara nyingine iliwakosa, Christopher Nkunku na Nicolas Jackson.
Pochettino awali alinukuliwa akisema kwamba wanafanya mapitio ya hali ilivyo katika kikosi baada ya kukiri hofu yake kuhusu Nkunku kutokuwa fiti.
Nkunku, nyota wa zamani wa RB Leipzig ya Ujerumani aliyesajiliwa Chelsea kwa ada ya Pauni 52 milioni, hadi sasa amecheza mechi nne tu za Chelsea tangu apate tatizo ya majeraha ya goti wakati wa maandalizi ya msimu.
Awali kulikuwa na habari kwamba Chelsea pia ilikuwa ikiisaka saini ya mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen na Ivan Toney wa Brentford lakini imeonekana kuna ugumu wa kuwapata wachezaji hao.
Akizungumzia habari hizo Pochettino alisema, “Hapna, nafikiri mnajua vizuri kwamba sizungumzii uvumi, siwezi katu kuwazungumzia wachezaji walio kwenye klabu nyingine, naliheshimu hilo.’
Badala yake Pochettino alisisitiza kwamba wanachofanya sasa ni mapitio ya kikosi chao na kama kuna kitakachotokea wataweka kila kitu wazi lakini kwa sasa hawajachukua uamuzi wowote.
Kimataifa Pochettino akana kusaka straika
Pochettino akana kusaka straika
Read also