Abidjan, Ivory Coast
Timu ya taifa ya Cameroon au ‘Indomitable Lions’ ina matumaini ya kumtumia nahodha wake Vincent Aboubakar (pichani) kwenye fainali za Afcon licha ya mchezaji huyo kupata matatizo ya misuli.
Vincent ambaye pia anaichezea Besiktas alipata matatizo ya misuli juzi Ijumaa na hapo hapo akaanza kupatiwa matibabu katika hospiali moja ya mjini Yamoussoukro nchini Ivory Coast.
“Wakati wa mazoezi ya Indomitable Lions mjini Yamoussoukro, nahodha wa timu ya taifa, Vincent Aboubakar alilazimika kuacha kufanya mazoezi baada ya kusikia maumivu kwenye misuli ya mguu wa kushoto,” alisema daktari wa timu hiyo, Patrick Fotso Gwabap.
“Hapo hapo mchezaji huyo alianza kufanyiwa matibabu na timu ya madaktari na baadaye kupelekwa hospitali kwa vipimo zaidi na kubaini ukubwa wa tatizo lake,”alifafanua zaidi Dk Gwabap.
“Hili ni tatizo dogo na haliwezi kumfanya akosekana au kumzuia mchezaji kushiriki mashindano,” alisema Dk Gwabap.
Aboubakar ambaye ana rekodi ya kubeba kiatu cha dhahabu katika fainali hizo mwaka 2022 nchini Cameroon baada ya kufunga mabao manane, hizi ni fainali zake za nne za Afcon.
Mchezaji huyo pia ndiye aliyeiwezesha Cameroon kubeba taji la Afcon mwaka 2017 mjini Libreville baada ya kufunga bao la dakika ya 88 katika mechi ya fainali dhidi ya Misri, mechi ambayo Cameroon ilitoka na ushindi wa mabao 2-1.
Kuna hofu kubwa kama nahodha huyo ataweza kucheza mechi ya kwanza ya Cameroon ya Kundi C dhidi ya Guinea itakayopigwa keshokutwa Jumanne au huenda akawa tayari kwa mechi ya pili dhidi ya Senegal itakayopigwa Ijumaa.
Baada ya mechi hizo, Cameroon itakamilisha mechi zake za hatua ya makunid dhidi ya Gambia, mechi itakayochezwa Januari 23.
Wakati huo huo, wenyeji Ivory Coast wameanza vyema fainali za Afcon Jumamosi hii kwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Guinea-Bissau.
Kimataifa Nahodha Cameroon hali tete
Nahodha Cameroon hali tete
Related posts
Read also