Na mwandishi wetu
Simba Queens imemrejesha kundini mshambuliaji, Jentrix Shikangwa (pichani) aliyekuwa anacheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya Beijing Jingtan ya China.
Mshambuliaji huyo raia wa Kenya msimu uliopita aliichezea Simba na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake akifunga mabao 25, anajiunga na Simba baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza na GreenSports leo Alhamisi, Meneja wa Queens, Seleman Makanya alisema wanaamini uwezo wa mshambuliaji huyo ndio maana wamemrudisha kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi chao ambacho kimelenga kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.
“Tuna imani naye ni mengi aliyafanya katika kipindi cha miezi sita kabla hajaenda China, tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu ambayo msimu huu inapambana kulirudisha taji la ligi kuu na kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa,” alisema Makanya.
Baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili, Jentrix huenda akaanza kuitumikia timu hiyo katika mchezo unaofuata ambao Simba Queens itacheza dhidi ya Amani Queens, Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Soka Jentrix arudi Simba Queens
Jentrix arudi Simba Queens
Read also