Na mwandishi wetu
Klabu ya Geita Gold FC inatarajia kuweka kambi ya wiki mbili mkoani Morogoro kujiandaa na michezo ijayo ya Ligi Kuu NBC sambamba na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Geita, Samwel Dida alisema hiyo ni baada ya kumalizika kwa mapumziko mafupi ya wiki mbili na sasa wanarudi kujipanga upya lengo likiwa ni kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
“Lengo la kuweka kambi mbali na nyumbani kwetu ni kumpa utulivu kocha wetu Denis Kitambi (pichani) kukaa na wachezaji wake na kuandaa silaha zake vizuri kabla ligi haijaendelea,” alisema Dida.
Kiongozi huyo alisema anaamini pia kutakuwa na maingizo mapya ya wachezaji kwenye dirisha dogo kutokana na mapendekezo ya kocha lakini kwanza wanapambana kutoka katika adhabu ya kufungiwa kutosajili kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Alisema wanakabiliwa na michezo migumu ya ligi dhidi ya Simba na Azam hivyo, hawana budi kuanza mipango mapema na kukiandaa vyema kikosi chao ili kupata matokeo mazuri.
Soka Geita kuweka kambi wiki mbili
Geita kuweka kambi wiki mbili
Read also