Manchester, England
Winga wa Manchester United, Jadon Sancho huenda akarudi katika klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund kwa mkopo baada ya kukataa kumuomba radhi kocha wake, Erik ten Hag.
Sancho alikataa kumuomba radhi Ten Hag baada ya kauli aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii akimpinga kocha wake baada ya timu hiyo kupoteza mechi yake na Arsenal, Septemba mwaka jana.
Ten Hag alisema kwamba mchezaji huyo aliwekwa kando katika mechi hiyo kutokana na kiwango chake kuwa chini mazoezini jambo ambalo Sancho hakukubaliana nalo na kuamua kumjibu kupitia mitandao ya kijamii.
Katika hoja yake, Sancho, 23, alisema kwamba alichokifanya kocha wake ni kumtoa kafara na tangu atoe kauli hiyo amekuwa akifanya mazoezi peke yake na hakuna dalili zozote za kurudishwa kikosi cha kwanza.
Man United ilimnunua Sancho Julai 2021 kutoka Dortmund kwa ada ya Pauni 73 milioni na zipo habari kwamba klabu hiyo ya Ujerumani ipo tayari kumrudisha mchezaji huyo katika kipindi hiki cha usajili cha Januari.
Ten Hag aliwahi kusema kwamba hatma ya Sancho katika kikosi cha Man United anayo Sancho mwenyewe lakini kinachoonekana ni kwamba winga huyo wa England ameamua kushikilia msimamo wa kutomuomba msamaha kocha wake.
Kimataifa Sancho kuuzwa Dortmund kwa mkopo
Sancho kuuzwa Dortmund kwa mkopo
Read also