Na mwandishi wetu
Coastal Union ya Tanga inayonolewa na kocha David Ouma (pichani) imeendelea na timuatimua ya wachezaji katika dirisha hili dogo la usajili baada ya kuwaacha wachezaji wengine watatu akiwamo kiungo wa kati, Abdulswamad Kassim.
Sambamba na kiungo huyo wa zamani wa Simba, wachezaji wengine wawili ambao nao hawatakuwa katika timu hiyo ya Ouma ni pamoja na Daud Mbweni na Yakubu Abdallah.
Kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kuhusiana na Abdulswamad, Coastal ilieleza: “Kiungo mkabaji bora, mshambuliaji pia na mwenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na akili ya zaida ni vitu ulivyojaaliwa, ila muda si rafiki. Tunasikitika muda ndio umeamua, tuseme asante.”
Abdulswamad alitua Coastal mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mlandege ya Zanzibar aliyoisaidia kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi msimu uliopita.
Kabla ya hapo kiungo huyo aliitumikia Simba kabla ya kutimkia Ruvu Shooting alikodumu kwa miezi sita na kutua Mlandege.
Baada ya tamko hilo, Coastal sasa imeachana na jumla ya wachezaji sita baada ya hivi karibuni kutangaza kuachana na Balama Mapinduzi, Juma Mahadhi na Fran Golubic.
Soka Coastal ya Ouma yaacha wengine watatu
Coastal ya Ouma yaacha wengine watatu
Read also