London, England
Arsenal leo Alhamisi inaumana na West Ham katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu England EPL) huku ikisaka matokeo yatakayoifanya imalize mzunguko huo ikiwa kileleni.
Kocha Mikel Arteta na vijana wake wanaelewa kuwa matokeo ya sare au kushindwa ni mwanzo wa tukio baya la kuibua maswali kwa kumaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya pili.
Ni tukio lnaloweza kukumbusha yaliyojiri msimu uliopita ambapo timu hiyo ilifanikiwa kushika usukani katika mzunguko wa pili kwa tofauti kubwa ya pointi kabla ya kuanza kupoteza mechi kimaajabu na kujikuta ikiliachia taji la EPL likielekea Man City.
Kumaliza mzunguko wa kwanza nafasi ya pili hakutoi dalili njema kwa timu ambayo kama ilivyokuwa msimu uliopita ilipewa nafasi kubwa ya kubeba taji la EPL kabla mambo hayajavurugika na msimu huu haitokuwa jambo jema mambo kuanza kuharibika mapema.
Msimu huu mzunguko wa kwanza pia unaweza kuhusishwa na tukio hilo la kupoteza taji katika hatua za mwisho hivyo Arsenal ina kila sababu ya kutoka uwanjani na ushindi mbele ya West Ham na kuhitimisha mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni.
Liverpool kwa sasa ndiyo inayoshika usukani EPL ikiwa imekamilisha mechi zake 19 za mzunguko wa kwanza kwa kujikusanyia pointi 42 dhidi ya 40 za Arsenal hivyo inachotakiwa kufanya Arsenal leo ni kutoka uwanjani na ushindi.
Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool, hakuuanza msimu huu vizuri, timu yake iliyumba kabla ya kutulia na kuanza kujikusanyia pointi ambazo hatimaye zimewafanya wamalize mzunguko wa kwanza vizur wakiwa kileleni.
Kwa jinsi msimamo wa EPL ilivyo hadi sasa ni timu hizo mbili tu za Arsenal na Liverpool ndizo zenye nafasi ya kumaliza mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa zikiwa kileleni jambo ambalo ni mwanzo wa dalili njema za kumalizia vizuri mechi nyingine 19 zilizobaki za kukamilisha mzunguko wa pili.
Liverpool hadi sasa wamelifanikisha hilo na Arsenal nao wanalitaka jambo hilo lakini mbele yao kuna mtihani wa West Ham ambao ni lazima waushinde kwanza.
Mechi za EPL leo Alhamisi, Desemba 28
Brighton v Tottenham
Arsenal v West Ham
Matokeo ya mechi za EPL jana Jumatano Desemba 27
Brentford 1-4 Wolves
Chelsea 2-1 Crystal Palace
Everton 1-3 Man City
Msimamo Top Ten EPL
P GD Pts
1 Liverpool 19 23 42
2 Arsenal 18 20 40
3 Aston Villa 19 15 39
4 Man City 18 22 37
5 Tottenham 18 13 36
6 Man Utd 19 -4 31
7 West Ham 18 1 30
8 Newcastle 19 12 29
9 Brighton 18 3 27
10 Chelsea 19 2 25
Kimataifa Arsenal kuiengua Liverpool kileleni EPL?
Arsenal kuiengua Liverpool kileleni EPL?
Read also