Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kutangazwa wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika na mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga (pichani) alisema wanaunda timu hiyo wanatoka mashindano ya Bingwa wa Mabingwa yaliyofanyika mkoani Iringa kuanzia Desemba 17-19, mwaka huu.
Alisema katika mashindano ya Bingwa wa Mabingwa uzani wa kg 48, Abdalah Maganga (MMJKT) alimshinda Mtemi Ramadhani (Ngome) kwa pointi na uzani wa kg 51 Iddi Athumani (MMJKT) alimshinda Haji Kudra (MMJKT) kwa pointi.
Uzani wa kg 54 Azizi Chala (Ngome) alimshinda Kaim Said (MMJKT) kwa pointi, kg 57 Stephano Mika (MMJKT) alimshinda John Dominick (Ngome) kwa pointi na kg 60 Hassani Mrutu (Ngome) alimshinda Mwarami Salum.
Katika kg 63.5, King Lucasi (Ngome) alimshinda Sikudhani Simon (Ngome) kwa pointi, kg 67 Addalah Mfaume (Ngome) alimshinda Elias Damson (MMJKT) kwa pointi, kg 71 Joseph Philipo (MMJKT) alimshinda Atanasi Ndiganya (Ngome), kg 75 Eliankunda Daniel (MMJKT) alimshinda Alphonce Abel (MMJKT) kwa pointi.
Katika kg 80 Juma Thabiti (Iringa) alimshinda Kevin Malya (Iringa) kwa pointi., kg 86 Mussa Wambura (Ngome) alishinda kwa W/O baada ya kutopata mpinzani, kg 92 Muhina Moriss (Ngome) alimshinda Fidelis Matonyinga (MMJKT) kwa pointi.
Kwa upande wa wanawake katika kg 52, Aisha Iddi alimshinda Latifa Oloki kwa pointi na Rachel Peter alipewa ushindi wa mezani baada ya kutopata mpinzani.
Pia ulichezwa mchezo wa makocha ambapo Mzonge Hassani (kocha Ngome) alicheza na John Selenge (kocha MMJKT) na matokeo kuwa sare katika uzani wa kg 92.
Ngumi Mabondia ngumi za ridhaa kutajwa wiki ijayo
Mabondia ngumi za ridhaa kutajwa wiki ijayo
Read also