Nyon, Switzerland
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), Man City wataumana na FC Copenhagen katika hatua ya mtoano au 16 bora ya ligi hiyo baada ya droo ya hatua hiyo kutangazwa leo Jumatatu.
Washiriki wengine wa hatua hiyo kutoka England, Arsenal ambao kwa sasa ndio wanaoshika usukani kwenye Ligi Kuu England wao wamepangwa kuumana na FC Porto ya Ureno, mechi ambazo mshindi anakwenda moja kwa moja hatua ya robo fainali.
Arsenal bado ina kumbukumbu ya kipigo cha mabao 5-0 ambacho iliipa Porto timu hizo zilipokutana kwa mara ya mwisho kwenye Uwanja wa Emirates mwaka 2010.
Kwa Conpenhagen ambao katika hatua ya makundi walikuwa kundi moja na Man United iliyoshindwa kusonga mbele, hii ni mara yao ya kwanza kucheza hatua hiyo tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2011.
Mechi za kwanza za hatua hiyo ambazo Man City na Arsenal zitakuwa ugenini, zitapigwa kati ya Februari 13 na 14 wakati za marudiano ambazo zitatoa washindi wa kufuzu robo fainali zitapigwa kati ya Machi 5 na 6 au Machi 12 na 13.
Timu zote kwa ujumla zimepangwa kama ifuatavyo…
Porto v Arsenal
Napoli v Barcelona
Paris St-Germain v Real Sociedad
Inter Milan v Atletico Madrid
PSV Eindhoven v Borussia Dortmund
Lazio v Bayern Munich
Copenhagen v Manchester City
RB Leipzig v Real Madrid
Europa Ligi
Feyenoord v Roma
Lens v Freiburg
Benfica v Toulouse
Galatasaray v Sparta Prague
AC Milan v Rennes
Young Boys v Sporting Lisbon
Sporting Braga v Qarabag
Shakhtar Donetsk v Marseille
Europa Conference Ligi
Sturm Graz v Slovan Bratislava
Servette v Ludogorets
Union Saint-Gilloise v Eintracht Frankfurt
Real Betis v Dinamo Zagreb
Olympiakos v Ferencvarosi
Ajax v Bodo/Glimt
Molde v Legia Warsaw
Maccabi Haifa v Gent