Na mwandishi wetu
Bonanza la Ujirani Mwema liloandaliwa na kudhaminiwa na Shamba la Miti la Sao Hill (Sao Hill Sport Bonanza) litafikia tamati kesho Jumamosi Desemba 16 kwa mechi ya soka ya fainali kati ya Ihefu FC na Mgololo Misitu.
Mechi hiyo ya soka pamoja na michezo mingine itachezwa kwenye makao makuu ya shamba la Miti la Sao Hill (Mafinga) Mufindi.
Timu 32 kutoka vijiji vyote vinavyozunguka msitu wa Shamba la Sao Hill kupitia tarafa nne ambazo ni Irundi, Ihefu, Ihalimba na Mgololo, zimeshiriki michuano hiyo kuanzia Desemba 9 mwaka huu.
Mbali na mechi hiyo ya soka pia kutakuwa na michezo mingine itakayopamba Bonanza hilo ambayo ni kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, kucheza bao na draft, mashindano ya kula, riadha na kucheza muziki.
Pia kutakuwa na mechi za veterans toka Igowele na Misitu FC huku kauli mbiu ya mashindano hayo ikiwa ni Panda Miti Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Soka Fainali Sao Hill Sport Bonanza Jumamosi
Fainali Sao Hill Sport Bonanza Jumamosi
Read also