Manchester, England
Man United huenda ikamkosa beki wake Raphael Varane ambaye anatajwa kuwa na mpango wa kuihama timu hiyo yenye makazi yake Old Trafford akiwa mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kukamkilika.
Habari za ndani zinadai kuwa mchezaji huyo hafurahii maisha ya Man United ikidaiwa kuwa picha haziendi na kocha wake Erik ten Hag na kwa muda mrefu amekuwa akipiga hesabu za kuondoka katika timu hiyo.
Mkataba wa Varane na Man United unatajwa kufikia mwisho majira ya kiangazi au kabla ya hapo, hivyo huenda Man United ikamkosa mchezaji huyu bila kupata chochote kama ataondoka akiwa huru.
Mambo si mazuri kwa sasa ndani ya kikosi cha Man United ambapo kocha wa timu hiyo, Ten Hag anapitia kipindi kigumu hasa baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baadhi ya wachezaji akiwamo Varane inadaiwa hawafurahii mambo yanavyokwenda chini ya himaya ya Ten Hag ikiwamo mfumo wake wa kuiongoza timu pamoja na mbinu anazotumia.
Varane, 30, beki ambaye pia ametamba kwa muda mrefu katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha kwanza cha Man United hivyo suala la kuondoka katika timu hiyo ni jambo ambalo limekuwa likizungumzwa sana katika siku za karibuni.
Kimataifa Varane ajipanga kuondoka Old Trafford
Varane ajipanga kuondoka Old Trafford
Read also