Montevideo, Uruguay
Mshambuliaji wa zamani wa Barca na Liverpool, Luis Suarez (pichani) ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay kitakachoivaa Argentina keshokutwa Alhamisi katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Suarez mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anaichezea Gremio ya Brazil ndiye mfungaji bora wa ligi ya Brazil Serie A akiwa na mabao 14 katika mechi 29 na anajiandaa kuivaa Argengtina ya Lionel Messi.
Baada ya mechi hiyo itakayopigwa mjini Buenos Aires, Suarez na timu yake ya Uruguay wataingia uwanjani tena kuivaa Bolivia siku tano baadaye.
Argentina ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia wanaongoza Kundi la Marekani Kusini katika mbio za kufuzu Kombe la Dunia wakiwa na pointi 12 katika mechi nne.
Mechi ya Argentina na Uruguay itawakutanisha Messi na Suarez ambao waliwahi kuwa pamoja katika klabu ya Barca huku Suarez akiwa njiani kuungana tena na Messi katika klabu ya Inter Miami FC ya Marekani.
Kocha wa Gremio, Renato Gaucho alithibitisha kuwa Suarez ataondoka katika klabu hiyo Desemba mwaka huu licha ya kwamba ndio kwanza yuko nusu ya mkataba wake wa miaka miwili aliousaini mwaka 2022.
Suarez amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Inter Miami huku mkataba huo ukiwa na kipengele kinachompa fursa ya kuongeza mwaka mwingine mmoja kama atakuwa tayari kufanya hivyo.
Kikosi kamili cha Uruguay, makipa: Sergio Rochet (Internacional), Franco Israel (Sporting Lisbon), Santiago Mele (Junior Barranquilla)
Mabeki: Ronald Araujo (Barca), José María Giménez (Atletico Madrid), Sebastián Cáceres (America), Matías Viña (Sassuolo), Bruno Méndez (Corinthians), Guillermo Varela (Flamengo) na Mathías Olivera (Napoli).
Viungo: Manuel Ugarte (Paris Saint-Germain), Rodrigo Bentancur (Tottenham), Federico Valverde (Real Madrid), Felipe Carballo (Gremio), Agustín Canobbio (Athletico Paranaense), Nicolás de la Cruz (River Plate), Giorgian de Arrascaeta (Flamengo), Facundo Pellistri (Manchester United), Maximiliano Araújo (Toluca) na Facundo Torres (Orlando City)
Washambuliaji: Cristian Olivera (Los Angeles FC), Federico Viñas (Leon), Darwin Núñez (Liverpool) na mkongwe Luis Suárez (Gremio)
Kimataifa Luis Suarez aitwa kikosini Uruguay
Luis Suarez aitwa kikosini Uruguay
Related posts
Read also