Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amewaomba Wanasimba kuacha kunyoosheana vidole na kupeana lawama, badala yake waungane ili kurejea katika ari ya ushindani wanayopaswa kuwa nayo.
Chama ameeleza hayo leo Alhamisi, saa chache kabla ya timu hiyo kuumana na Namungo ya Lindi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kiungo huyo ameeleza hayo zikiwa zimepita siku nne tangu wachezee kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa mahasimu wao, Yanga hali iliyoibua tafrani na kuondoshwa kwa kocha wao, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ huku baadhi ya wachezaji wakitupiwa lawama wakidaiwa kuhusika kuizorotesha timu hiyo siku hiyo.
“Katika nyakati hizi hakuna haja ya kunyoosheana vidole na kutupiana lawama, haitotusaidia kwa namna yoyote ile. Huu ni wakati sahihi wa kushikamana pamoja na kuunganisha nyoyo zetu. Twendeni tena leo tukiwa na nguvu moja na kufanyabkazi ili kurejea katika ari yetu,” aliandika Chama katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Kipigo cha Jumapili kilichafua rekodi ya timu hiyo ya kutofungwa kwenye michuano yoyote tangu kuanza kwa msimu huu lakini pia kushindwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi na kuiacha Yanga ikijitanua kwa pengo la pointi sita kabla ya Wekundu hao kushuka dimbani leo.
Soka Chama: Tusinyoosheane vidole
Chama: Tusinyoosheane vidole
Read also