Manchester, England
Man United inadaiwa kutaka kumrudisha aliyekuwa kipa wake, David de Gea kwa kumpa mkataba wa muda mrefu ikiwa ni miezi minne tangu imruhusu kipa huyo aondoke.
De Gea aliondoka katika klabu hiyo baada ya mabosi wake kutokuwa tayari kumpa mkataba mpya kwa kile kilichodaiwa kwamba kipa huyo alikuwa akitaka maslahi makubwa.
Baada ya kuondoka kwa De Gea, Man United ilimsajili aliyekuwa kipa namba moja wa Inter Milan, Andre Onana ambaye hata hivyo amekuwa katika lawama kwa makosa yaliyoigharimu timu hiyo kwenye mechi kadhaa.
Katika kuhakikisha wanakuwa na kipa mahiri, macho yameelekezwa kwa De Gea ambaye kuondoka kwake Man United kuliacha maswali ingawa kilichokuwa wazi ni kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alikataa kusaini mkataba mpya.
Onana ambaye amekuwa lawamani hata hivyo katika mechi mbili zilizopita ameonekana kuwa kama mwenye kurudi katika ubora wake hasa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen.
Katika mechi hiyo, Onana mbali na kuokoa michomo kadhaa, kipa huyo pia aliokoa penalti na kuifanya timu yake itoke na ushindi wa bao 1-0, ushindi ambao umefufua matumaini mapya kwa timu hiyo baada ya kuwa katika kipindi kigumu.
Kimataifa Man United kumrudisha De Gea
Man United kumrudisha De Gea
Read also