Zurich, Switzerland
Morocco, Hispania zimepitishwa kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia *WC) 2030 pamoja na Ureno lakini zipo dalili za kuibuka utata baada ya nchi zote hizo kila moja kutaka uenyeji wa mechi ya fainali.
Waziri wa Michezo wa Hispania, Miquel Iceta ametoa kauli inayoonesha dalili za Hispania kuwa mwenyeji wa mechi hiyo akisema hayo ndiyo matarajio yake ingawa alisema huwezi kutegemea kupata kifaranga kabla ya yai kutotolewa.
Kwa upande wake kiongozi wa timu ya Morocco kutoka Shirikisho la Soka Morocco, Fouzi Lekjaa alisema kwamba lengo lao ni kuona mechi ya fainali ikichezwa katika jiji la Casablanca.
Alisema ana matumaini ya kuona juhudi za nchi hiyo zikilipa kwa uwezo wa Mungu akiamini kwamba fainali ya kihistoria itachezwa katika uwanja wa mjini Casablanca.
Fifa ilitangaza juzi Jumatano kuzipa nchi za Morocco, Hispania na Ureno uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2030 na Uruguay, Argentina na Paraguay kuwa wenyeji wa mechi tatu ambazo zitakuwa maalum kwa kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa fainali za Kombe la Dunia.
Argentina nayo kwa upande wake baadhi ya maofisa wa serikali ya nchi hiyo wanadaiwa kusema kwamba nchi hiyo itaangalia uwezekano wa kuongezewa mechi nyingine badala ya mechi moja ya ufunguzi.
Lekjaa alisema kwamba nchi za Morocco, Ureno na Hispania zitakutana Oktoba 18 mjini Rabat kujadiliana kuhusu mechi za Kombe la Dunia ambapo nchini Morocco miji sita itakuwa na viwanja vya mechi hizo.
Kombe la Dunia Nani mwenyeji mechi ya fainali WC 2030?
Nani mwenyeji mechi ya fainali WC 2030?
Read also