Manchester, England
Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa winga wake, Antony anatarajia kurudi mazoezini ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu ahusishwe na tuhuma za udhalilishaji kijinsia.
Antony, 23, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, jana Alhamisi aliripoti kituo cha polisi jijini Manchester na baada ya kuhojiwa hakuwekewa vikwazo vyovyote na hajakamatwa au kushitakiwa Uingereza au Brazil.
Taarifa ya Man United iliyopatikana leo Ijumaa ilieleza, “Antony ni mwajiriwa wa Manchester United na imeamriwa ataendelea na mazoezi na anaweza kucheza mechi wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea. Hili litakuwa likifanyiwa mapitio wakati taratibu nyingine zikiendelea.”
Hata hivyo haitarajiwi mchezaji huyo kuanza mazoezi leo Ijumaa au kupata nafasi ya kucheza mechi ya kesho Jumamosi ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace itakayopigwa Old Trafford.
Hadi sasa Antony ameshakosa mechi nne za Man United tangu apewe likizo inayoandamana na malipo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake na wanawake watatu akiwamo rafiki na mpenzi wake wa zamani, Gabriela Cavallin.
Septemba 4 mwaka huu chanzo kimoja cha habari nchini Brazil kiliripoti tuhuma zilizotolewa na Gabriella akilalamika kupigwa kichwa na Antony katika hoteli moja mjini Manchester, tukio analodaiwa kulifanya Januari 15 mwaka huu.
Mwanadada huyo pia alidai kwamba Antony alimpiga ngumi kifuani na kumsababishia maumivu makubwa.
Tuhuma nyingine dhidi ya Antony ziliwasilishwa na wasichana wengine wawili, Rayssa de Freitas na Ingrid Lana kila mmoja akidai kwamba mwaka 2022 alipigwa na Antony ingawa mchezaji huyo ambaye pia aliondolewa katika kikosi cha Brazil, amekana tuhuma zote hizo.
Kimataifa Antony kurejea mazoezini Man United
Antony kurejea mazoezini Man United
Read also