Na mwandishi wetu
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta amefungua akaunti ya mabao katika timu yake mpya ya PAOK Thessaloniki ya Ugiriki akiiongoza kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Volos NFC.
Samatta aliyejiunga na PAOK msimu huu akitokea Fenerbahçe ya Uturuki alifunga bao hilo dakika ya 55 katika mchezo wa Ligi Kuu Ugiriki kabla ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 81, nafasi yake ikichukuliwa na Stefanos Tzimas.
Mabao mengine yalifungwa na Konstantinos Koulierikas dakika ya 39 na Thomas Murg aliyetupia dakika ya 45 katika mchezo huo uliopigwa jana Jumatano kwenye Uwanja wa Toumba, Thessaloniki.
Samatta mchezaji wa zamani wa Aston Villa ya England amefunga bao hilo baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi nne za awali kati ya tano za ligi alizoitumikia timu hiyo mpaka sasa.
PAOK inashika nafasi ya pili kati ya timu 14 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 dhidi ya pointi 16 za vinara Olympiacos, baada ya wote kucheza mechi sita.
Kimataifa Samatta aanza kutupia PAOK
Samatta aanza kutupia PAOK
Read also