Na mwandishi wetu
Wachezaji wa Simba wa kimataifa Henock Inonga na Aubin Kramo waliokuwa majeruhi wamerejea kwenye kikosi hicho tayari kwa mashindano yaliyoko mbele yao.
Inonga aliumia katika michuano ya Ngao ya Jamii mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Big Stars na kukosa mchezo wa fainali dhidi ya Yanga na michezo miwili ya Ligi Kuu NBC.
Kramo ambaye hakuwahi kupata nafasi ya kuitumikia Simba tangu kusajiliwa kwake msimu huu ambapo awali ilielezwa anasumbuliwa na kuumwa mara kwa mara, sasa mambo yanakwenda vizuri.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alithibitisha kurejea kwa wachezaji hao na tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mashindano yote yaliyoko mbele yao.
“Wachezaji wetu wote majeruhi wamepona, Inonga alipewa wiki mbili za mapumziko na Kramo alipewa wiki moja baada ya majeraha aliyoyapata, sasa wameshapona na wamerejea kikosini,” alisema.
Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaochezwa ugenini Zambia Septemba 16, mwaka huu hivyo kurejea kwa wachezaji hao kunarejesha matumaini ya timu hiyo kuelekea katika mechi hizo.
Soka Inonga arejea kikosini Simba
Inonga arejea kikosini Simba
Read also