Sydney, Australia
Timu ya Wanawake ya England au Lioness imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Dunia Wanawake (WWC) kwa kuwalaza wenyeji Australia mabao 3-1 na sasa itaumana na Hispania Jumapili katika mechi itakayomtangaza bingwa wa dunia.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya soka ya England kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo ya soka mikubwa duniani tangu ifanye hivyo timu ya wanaume ambayo iliyofikia hatua hiyo mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1966 na hatimaye kubeba taji.
Kwa hali hiyo iwapo Lioness watafanikiwa kulibeba taji hilo watakuwa wamekifanya kile ambacho kilifanywa na timu ya wanaume mwaka 1966 kwa mara ya kwanza na ya mwisho.
Lioness pia wakifanikiwa kutwaa taji hilo itakuwa ni rekodi nyingine nzuri kwa timu hiyo ya wanawake baada ya kubeba Kombe la Ulaya (Euro 2022) katika fainali zilizofanyika England mwaka jana.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumatano hii, Lioness ilianza kuandika bao lake la kwanza katika dakika ya 36 lililofungwa na Ella Toone kwa shuti kali, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za kwanza.
Australia hata hivyo walipambana hasa katika kipindi cha pili na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 63 kwa bao la Sam Kerr ambaye alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza tangu kuanza fainali hizo.
England hata hivyo walipambana baada ya kuingia kwa bao hilo na kupata bao la pili dakika ya 71 mfungaji akiwa ni Lauren Hamp aliyeyatumia makosa ya mabeki wa Australia kabla Alessia Russo hajamalizia kwa bao la tatu katika dakika ya 86.
Kombe la Dunia Ni England, Hispania fainali Kombe la Dunia
Ni England, Hispania fainali Kombe la Dunia
Read also