Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Muhene ‘Try Again’ amehudhuria kozi ya Diploma ya Uongozi wa Klabu jijini Sydney, Australia na kupata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Fifa, Gianni Infantino.
Katika mazungumzo na kiongozi huyo wa soka duniani, jambo kubwa walilojadili ni kuhusu michuano ya Africa Super League pamoja maendeleo ya soka nchini Tanzania.
Kupitia mtandao wa Simba, Try Again amesema Infantino amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika huku akiipongeza pia Tanzania kwa jinsi ambavyo soka lake linazidi kupanda siku hadi siku.
“Nimefurahi kukutana na Rais wa Fifa, Infantino pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, Ornella Desirée Bellia kujadili kuhusu Super League. Majadiliano yamekuwa mazuri na jambo jema Rais Infantino anaielewa vizuri Tanzania na ameniahidi atakuwepo kwenye uzinduzi wa Super League ambao utafanyika Tanzania.
“Tuko hapa Sydney kushiriki kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na Fifa lakini pia kufanya shughuli za mpira ikiwemo kujifunza namna mashindano makubwa yanavyoandaliwa kama Kombe la Dunia la Wanawake ambalo linafanyika hapa Australia na New Zealand.
“Kama mnavyofahamu Simba itashiriki katika Africa Super League hivyo uzoefu huu utatusaidia katika uandaaji wa sherehe za ufunguzi pamoja na michezo ya kimataifa iliyopo mbele yetu,” alisema Try Again.
Kimataifa Try Again ateta na Rais wa Fifa
Try Again ateta na Rais wa Fifa
Read also