Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba leo Jumamosi imemtambulisha kipa Ayoub Lakred, kutoka FAR Rabat ya Morocco aliyesaini mkataba wa miaka miwili na Wekundu hao.
Kipa huyo, 28 anatarajiwa kuwa kipa namba moja kuchukua nafasi ya Aishi Manula ambaye kwa sasa anauguza maumivu ya goti yanayotarajiwa kumuweka nje ya uwanja hadi Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na GreenSports, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema kocha wao, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alihitaji kipa mwingine mwenye uzoefu na mashindano ya kimataifa.
“Ayoub ni chaguo sahihi kwetu, rekodi zake kwenye mashindano ya kimataifa ni nzuri lakini pia ana uzoefu mkubwa hivyo naamini atatusaidia katika mashindano yote ambayo Simba tutashiriki msimu huu,” alisema Ahmed.
Akizungumzia mustakabali wa makipa wazawa Hussein Abel ambaye amesajiliwa hivi karibuni kutoka KMC, Ally alisema kipa huyo ataendelea kubaki Simba kupigania nafasi ya kucheza.
Mbali na makipa hao, Simba pia ina kipa kinda, Ally Salim aliyeanza kudaka kikosi cha kwanza mwishoni mwa msimu uliopita na kuiwakilisha timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Salim pia majuzi aliibuka shujaa kwa kupangua penalti katika mechi dhidi ya Singida Fountain Gate na kuisaidia Simba kutinga fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 4-2 na Jumapili hii itaumana na Yanga.
Soka Kipa wa FAR Rabat atua Simba
Kipa wa FAR Rabat atua Simba
Read also