Sydney, Australia
Mshambuliaji wa timu ya wanawake ya England, Lauren James ameomba radhi baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria akisema atajifunza kutokana na kosa hilo.
Lauren alipewa kadi hiyo na kutoka nje baada ya kumkanyaga makusudi Michelle Alozie wa Nigeria katika mechi ambayo hatimaye England iliibuka na ushindi wa penalti 4-2 na kukata tiketi ya robo fainali.
Kwa kupewa kadi hiyo, Lauren ambaye pia alimuomba radhi Michelle kupitia mitandao ya kijamii, ataikosa mechi ya robo fainali dhidi ya Nigeria. “Mapenzi yangu na heshima kwako, samahani kwa kilichotokea,” alisema akimwambia Michelle.
Lauren pia aliwaomba radhi mashabiki wa England na wachezaji wenzake. “Pia kwa mashabiki wetu wa England na wachezaji wenzangu, kucheza nikiwa nanyi ni heshima kubwa na nawaahidi kujifunza kutokana na kilichotokea,” alisema.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alikuwa mmoja wa wachezaji nyota wa timu hiyo katika mechi za hatua ya makundi akiwa amefunga mabao matatu na kutoa asisti tatu na tayari maofisa wa timu ya England nao wametoa taarifa ya kumuunga mkono kwa namna alivyoomba msamaha.
Na ingawa inaelezwa kwamba atakosa mechi moja lakin Fifa hawajatoa taarifa rasmi ya idadi ya mechi ambazo mchezaji anaweza kukosa akiwa na kadi nyekundu hivyo Lauren anaweza kukosa mechi za hatua inayofuata kama England itasonga mbele.
Kombe la Dunia Mshambuliaji England aomba radhi
Mshambuliaji England aomba radhi
Read also