Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 51 milioni kwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah wakati huo huo kukiwa na habari kuwa kiungo wa Man City, Kevin de Bruyne (pichani) naye anatakiwa nchini humo.
Salah mwenye umri wa miaka 31, klabu ya Al-Ittihad ambayo pia imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema, inadaiwa kumuandalia Salah mkataba wa miaka miwili na malipo yanayofikia Pauni 155 milioni katika kipindi hicho.
Kuhusu De Bruyne mwenye umri wa miaka 32 ofa yake haijawekwa wazi lakini yumo katika hesabu za klabu hiyo kuhakikisha naye anaiacha Ligi Kuu England (EPL) na kuhamia Ligi Kuu Saudi Arabia.
Ikitokea mpango wa Salah kwenda Saudi Arabia utafanikiwa, mchezaji huyo pia atakuwa anaungana na nyota mwenzake wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane ambaye msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Mane amejiunga na Al-Nassr akitokea Bayern iliyomsajili kutoka Liverpool kabla ya kuanza msimu wa 2022-23. Winga wa zamani wa Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo naye anaichezea timu hiyo
Kwa Salah ambaye pia ni mshambuliaji nyota wa timu ya Taifa ya Misri, hii itakuwa ofa ya pili kumtaka atoke Liverpool kwani PSG ya Ufaransa nayo inamtaka ikisubiri pesa za mauzo ya Kylian Mbappe ili iwe na jeuri ya kumnunua Salah.
Mpango wa De Bruyne ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ubelgiji, haujawekwa wazi zaidi ya kuwapo habari kuwa naye yumo kwenye hesabu za wachezaji wanaotakiwa kuinogesha ligi ya Saudi Arabia.
Kimataifa De Bruyne, Salah haooo Saudi Arabia
De Bruyne, Salah haooo Saudi Arabia
Read also