London, England
Mmiliki wa klabu ya Tottenham Hotspur, Joe Lewis amemwambia mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy kuwa lazima amuuze mshambuliaji wao, Harry Kane kama hawezi kumshawishi asaini mkataba mpya.
Kauli hiyo ya Lewis inazidi kuipa nguvu Bayern Munich ambayo imekuwa ikimtaka mshambuliaji huyo ingawa Man United ambayo awali ilitangaza kutomtaka tena mshambuliaji huyo nayo inadaiwa kubadilika baada ya kuona kuna matumaini mapya.
Man United iliwahi kutangaza kujitoa katika mbio za kumtaka Kane na kuiacha Bayern ikiendelea na harakati hizo na tayari ofa zake mbili zimeshakataliwa na Levy ambaye anataka kuvuna pesa ndefu.
Wakati Levy akiwa katika mkakati wa kuvuna pesa, Lewis ameingia hofu kwa imani kwamba iwapo watashindwa kumuuza ataondoka baada ya msimu wa 2023-24 bila ya wao kupata chochote kwa kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Spurs unafikia ukomo mwakani.
Mazingira hayo sasa yanaibua vita mpya kati ya Bayern na Man United kila klabu ikiamini inaweza kumpata mshambuliaji huyo ambaye pia amewahi kusema kwamba anataka kuondoka Spurs ili kusaka changamoto mpya na aliwahi kukataa kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.
Ukiachana na Man United na Bayern, PSG nayo imewahi kutangaza kumtaka Kane ambaye pia aliwahi kusema kwamba angependa kwenda Bayern na si PSG ingawa Spurs inaweza kushawishika kumuuza katika klabu yoyote itakayowasilisha ofa nono.
Real Madrid nayo ni klabu nyingine ya mwanzo mwanzo kuonesha nia ya kumtaka Kane, nayo bila shaka kauli ya Lewis inaweza kuwaibua upya wakijiaminisha kumpata mshambuliaji huyo.
Kimataifa Kigogo Spurs ataka Kane auzwe
Kigogo Spurs ataka Kane auzwe
Read also