London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na yuko wazi katika mpango wake wa kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani.
Kane mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo na nahodha wa timu ya Taifa ya England, atakuwa tayari kuondoka kama Spurs itakubali ada ya uhamisho lakini hatolazimisha kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Msimamo huo wa Kane umekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu atangaze kwamba yuko tayari kujiunga na timu hiyo ya Ujerumani lakini hatokuwa tayari kuichagua PSG ambayo pia inamtaka.
Mkataba wa Kane na Spurs unafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao na kilichopo ni kwamba kama timu hiyo haitomuuza sasa itajikuta ikimshuhudia akiondoka bila ya wao kupata chochote pale atakapomaliza mkataba wake labda kama atabadili mawazo na kusaini mkataba mpya wakati huu.
Tayari Bayern imeshawasilisha ofa mbili ambazo zimekataliwa na Spurs hapo hapo kukiwa na habari kwamba Real Madrid ambayo pia inadaiwa kumtaka mshambuliaji huyo inafuatilia kwa karibu maendeleo hayo kabla ya kufanya maamuzi.
Kimataifa Kane agomea mkataba mpya Spurs
Kane agomea mkataba mpya Spurs
Read also