Na mwandishi wetu
Timu ya Geita Gold inatarajiwa kuweka kambi ya wiki tatu mkoani Morogoro kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu NBC utakaoanza Agosti 15, mwaka huu.
Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Geita, Samuel Dida alisema program za mazoezi zitaanza kesho Jumatano.
Alisema wamechagua kambi ya Morogoro kutokana na hali ya hewa nzuri lakini pia wanatarajia kucheza michezo kadhaa ya kirafiki kupitia mashindano maalum yatakayofanyika mkoani hapo.
“Tutakuwa na michezo ya kirafiki pale lakini pia kutakuwa na mashindano maalum ambayo tumealikwa, yatafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, na sisi ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki,” alisema.
Kwa mujibu wa Dida, watakaa Morogoro mpaka Agosti 3, kisha wataelekea nchini Rwanda kucheza michezo ya kirafiki dhidi ya klabu ya Mukulu wanaoadhimisha miaka 60 ambapo watakaa kwa siku mbili kisha waterejea Geita.
Alisema kabla ya kuanza msimu watafanya uzinduzi wa jezi kisha tamasha fupi la kutambulisha wachezaji wapya na kuwapongeza vijana wao waliofika hatua ya fainali kwenye ligi ya vijana.
Soka Geita Gold kuweka kambi Moro
Geita Gold kuweka kambi Moro
Read also