Switzerland
Klabu za Manchester United na Barcelona zimepigwa faini na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni inayohusu nidhamu ya matumizi fedha yaani Financial Fair Play (FFP).
FFP ni kanuni iliyoanzishwa na Uefa mwaka 2009 kwa lengo la kuzibana klabu zisitafute mafanikio kwa kufanya matumizi yanayozidi kile wanachoingiza jambo ambalo baadaye huharibu uimara wa uchumi katika klabu hizo.
Man United imetozwa faini ya Dola 336,420 kwa makosa waliyoyafanya katika mwaka wao wa fedha wa 2019 na 2022 wakati Barca imetozwa faini ya Dola 560,700 kwa makosa ya mwaka 2022.
Klabu za AC Milan, Inter Milan na Paris Saint-Germain (PSG) ambazo zote Septemba mwaka jana zilikumbana na adhabu ya Uefa kwa kanuni ya FFP, safari hii zimekidhidhi matakwa ya kanuni hiyo kwenye matumizi yao ya fedha msimu uliopita.
Uefa hata hivyo itaendelea kuzifuatilia kwa karibu klabu hizo ili kujua kama zitaendelea kufanya matumizi yao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya FFP.
Kanuni ya FFP ni miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kusimamiwa kwa nguvu zote na Rais wa sasa wa Uefa, Aleksandre Caferine (pichani juu).
Kimataifa Uefa yaziadhibu Barca, Man United
Uefa yaziadhibu Barca, Man United
Read also