Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa Kundi E ambalo pia lina timu za Morocco na Zambia katika kuwania kufuzu fainali ya Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika katika nchi za Mexico, Canada na Marekani.
Ili kufuzu fainali hizo, Stars itakuwa na kibarua kigumu cha kushika usukani wa kundi hilo na kuwa moja ya timu 48 zitakazoshiriki fainali hizo ambazo kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo, idadi ya timu shiriki itakuwa kubwa.
Stars ikishika usukani wa kundi itafuzu moja kwa moja, tofauti na hivyo inahitaji kukusanya pointi nyingi ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kuwania kufuzu kupitia mchujo dhidi ya timu pinzani ya bara jingine ambayo itapangiwa.
Katika mazingira hayo mtihani mkubwa kwa Stars ni timu ya Morocco kwani ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kushika usukani wa kundi hilo kutokana na ubora wa soka la nchi hiyo ambayo kwa mujibu wa rekodi za hivi karibuni za Fifa, nchi hiyo inashika nafasi ya 13 kwa ubora duniani.
Morocco pia katika fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar, iliweka rekodi ya kufikia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na hivyo kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufikia hatua hiyo.
Wapinzani wengine wa Stars katika kundi hilo ni timu ya Congo ambayo pia si ya kubeza lakini pia zipo timu za Niger na Eritrea ambazo zinakamilisha idadi ya timu sita za kundi hilo,
