Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu mpya wa Mashujaa, Mohamed Abadallah ‘Bares’ amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kwani anaisuka timu ya ushindani kwelikweli kuelekea msimu ujao.
Bares aliyechukua mikoba ya kocha Abdul Mingange amefafanua kuwa licha ya ugeni wa timu hiyo iliyopanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao lakini anaamini atawaandaa vilivyo wachezaji wake kuhakikisha wanapambania mno matokeo ya timu hiyo.
“Tupo kwenye maandalizi kiujumla, hatujaanza mazoezi lakini tunaendelea na michakato mingine ya usajili na vitu vingine muhimu kuhakikisha timu inakuwa nzuri na ngumu kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao.
“Wachezaji wengi wanafanana isipokuwa ni namna gani unawaandaa, hivyo tutawaandaa kiushindani na kuipa timu matokeo, tufanye vizuri na mashabiki pia wafurahi na waje kuangalia timu yao,” alisema Bares.
Mashujaa yenye maskani yake mkoani Kigoma, imepanda ligi kuu baada ya kuizamisha Mbeya City kwa jumla ya mabao 4-1 katika mechi mbili za mtoano za kuwania kushiriki ligi hiyo msimu ujao wa 2023-24.
Soka Bares awatoa hofu mashabiki Mashujaa
Bares awatoa hofu mashabiki Mashujaa
Read also