Manchester, England
Kipa David De Gea amesema kwamba huu ni wakati sahihi kwake kusaka changamoto mpya kwingineko akithibitisha kwamba anaondoka Man United, timu aliyoichezea kwa miaka 12.
De Gea mwenye umri wa miaka 32 mkataba wake na Man United unafikia ukomo mwishoni mwa mwezi huu na hivyo atakuwa mchezaji huru baada ya mpango wa kumuongezea mkataba kukwama.
“Ningependa kutuma salamu za kwaheri kwa mashabiki wote wa Man United,” aliandika kwenye mitandao ya kijamii kipa huyo aliyeichezea timu hiyo jumla ya mechi 545.
“Sasa ni wakati sahihi kukimbilia changamoto mpya, kujisogeza katika mazingira mapya, Manchester itaendelea kuwa moyoni mwangu, Manchester imenijenga na haiwezi kamwe kuniacha,” alisema.
De Gea ambaye ni raia wa Hispania, alijiunga na Man United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid kwa ada ya Pauni 18.9 milioni.
Kuondoka kwa De Gea kumekuja wakati kocha wa Man United, Erik ten Hag akiwa na matumaini makubwa ya kumsajili kipa wa Inter Milan, Andre Onana.
Habari za awali zinadai kwamba mpango wa kumuongezea mkataba De Gea ulioafikiwa awali baadaye ulibadilika na kuzifanya pande zote mbili kusimamisha mpango huo.
Kimataifa De Gea aaga Man United
De Gea aaga Man United
Read also