Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imemtambulisha straika mpya kutoka Senegal, Allasane Diao (pichani) aliyesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka US Goree inayoshiriki Ligi Kuu ya Senegal ametambulishwa na Azam jioni ya leo Jumanne kupitia mitandao yao ya kijamii.
Huo unakuwa usajili wa tatu kwa Azam kuelekea msimu ujao wakiendelea kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu NBC na Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam FC hivi karibuni ilifanikiwa kuinasa saini za viungo washambuliaji, Djibril Sillah kutoka Raja Casablanca na Feisal Salum au Fei Toto kutoka Yanga SC.
Klabu hiyo hivi karibuni inatarajiwa kwenda nchini Tunisia kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao.
Soka Azam FC yanasa straika mpya
Azam FC yanasa straika mpya
Read also