Na mwandishi wetu
Timu ya Simba imetangaza rasmi kuachana na kiungo wake wa kati, Victor Akpan (pichani) baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa msimu mmoja pekee.
Simba imeweka wazi hilo leo Jumanne kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya awali kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu ya wiki hii wataanza kuwataja wachezaji ambao hawatakuwa nao msimu ujao.
“Akpan alikuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao,” ilifafanua taarifa kwenye mtandao wa klabu ya Simba.
Akpan raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu wa 2022-23 akitokea Coastal Union alikoonesha kiwango cha kuvutia na kuisaidia Coastal kufika fainali ya Kombe la FA (ASFC) msimu wa 2021-22.
Hata hivyo, katikati ya msimu uliopita alitolewa kwa mkopo Ihefu na kuitumikia timu hiyo kwa miezi sita kabla ya Simba kumuonesha mlango wa kutokea.
Mpaka sasa Akpan anakuwa mchezaji wa pili wa kimataifa kuachwa na timu hiyo baada ya awali kutangaza kuachana na Augustine Okrah raia wa Ghana.
Soka Akpan aonyeshwa mlango Simba
Akpan aonyeshwa mlango Simba
Read also