London, England
Timu za Leicester na Leeds United zimeungana na Southampton kushuka daraja zikiaga rasmi Ligi Kuu England (EPL) baada ya mechi za leo Jumapili ambazo ni za mwisho huku Everton ikiepuka janga hilo.
Everton ambayo ilikuwa inachungulia kaburi, ushindi wa bao 1-0 ilioupata mbele ya Bournemouth umekuwa na maana kwa timu hiyo ambayo imefikisha pointi 36 ikishika nafasi ya 17 na hivyo kujihakikishia kucheza EPL msimu ujao.
Msimu wa EPL 2022-23 umehitimishwa rasmi kwa mechi za mwisho kuchezwa leo ambapo timu hizo tatu sasa zitacheza Ligi ya Champioship kuanzia msimu ujao wa 2023-24.
Southampton ambayo ilishaaga EPL siku chache zilizopita, imehitimisha mechi yake ya mwisho leo kwa sare ya mabao 4-4 na Liverpool na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 25 na ndiyo inayoshika mkia.
Timu ya Leeds ambayo nayo haikuwa katika nafasi nzuri imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 18 na pointi 31 na katika mechi ya leo imelala kwa mabao 4-1 mbele ya Tottenham.
Leicester, ambao ni mabingwa wa EPL msimu wa 2015-16, licha ya kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya West Ham, ushindi huo haukuweza kuwaokoa na janga hilo na wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya 19 na pointi zao 34.
Matokeo ya mechi zote za leo ambazo ni za mwisho kwa msimu wa EPL 2022-23 ni kama ifuatavyo…
Arsenal 5-0 Wolves
Aston Villa 2-1 Brighton
Brentford 1-0 Man City
Chelsea 1-1 Newcastle
Crystal Palace 1-1 Nottm Forest
Everton 1-0 Bournemouth
Leeds 1-4 Tottenham
Leicester 2-1 West Ham
Man Utd 2-1 Fulham
Southampton 4-4 Liverpool