Na mwandishi wetu
Yanga imeripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kumnasa mshambuliaji mahiri wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Chivaviro (pichani).
Mabingwa hao wa Ligi Kuu NBC wametajwa kumuhitaji mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 10 kwenye ligi na sita kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sawa na Fiston Mayele wa Yanga, baada ya kuelezwa kumkosa Khanyisa Mayo wa Cape Town City.
Mitandao mbalimbali ya Afrika Kusini imefafanua kuwa Yanga imeshapeleka ofa nono ambayo haikuwekwa wazi kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo ambaye timu yake imeshuka daraja juzi baada ya kufungwa mabao 2-0 na Swallows.
Na ingawa mabosi wa Marumo kuonekana kukubaliana na ofa hiyo lakini wanatarajia kukamilisha dili hilo wiki ijayo kama hakutakuwa na ofa nono zaidi kutoka kwa baadhi ya timu za nchi hiyo zinazomuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
Yanga iko kwenye mawindo ya mshambuliaji mpya baada ya kuendelea kusambaa kwa fununu kuwa Mayele anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu yakiwamo madai kwamba klabu kadhaa zinamuwania kutokana na kiwango anachokionesha mpaka sasa.
Awali, Yanga ilionesha kuvutiwa na Mayo anayeongoza orodha ya wafungaji kwa mabao 12 kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini, kabla ya hivi karibuni kuibuka kwa taarifa kuwa mshambuuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameongezewa mkataba wa miaka mitatu na timu yake hiyo.
Kimataifa Usajili wa Chivaviro Yanga wafika pazuri
Usajili wa Chivaviro Yanga wafika pazuri
Read also