Na mwandishi wetu
Simba haijakata tamaa na taji la Ligi Kuu NBC, ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Ruvu Shooting umeifanya ifikishe pointi 67, ushindi ambao utakuwa na maana kubwa kama Jumamosi itakuwa siku mbaya kwa Yanga mbele ya Dodoma Jiji.
Kwa ushindi huo, Simba inayoshika nafasi ya pili katika ligi hiyo, imeisogelea Yanga kwa tofauti ya pointi nne huku ikiombea matokeo mabaya katika mechi zilizobaki za timu hiyo kuanzia mechi na Dodoma Jiji Jumamosi hii.
Ushindi wa Simba uliopatikana Ijumaa hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex utabaki kuwa furaha ya Simba pekee na hautoisumbua Yanga kama timu hiyo itafanikiwa kuchota pointi zote tatu mbele ya Dodoma Jiji.
Mechi na Dodoma itakuwa ya 28 kwa Yanga kama ilivyo Simba na iwapo itashinda itatawazwa rasmi kinara wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2022/23 kwa kufikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Ikitokea Yanga itashindwa au kutoka sare mbele ya Dodoma Jiji, hapo itakuwa imejichelewesha katika kutawazwa kinara wa ligi na kuzidi kufufua matumaini ya Simba ambayo kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mgunda hivi karibuni alinukuliwa akisema kwamba bado hawajakata tamaa katika mbio za kulisaka taji hilo hadi mwisho utakapofika.
Simba katika mechi na Dodoma ilianza kuhesabu mabao yake katika dakika ya 29 mfungaji akiwa Clatous Chama kabla ya Pape Sakho kuhitimisha mabao mawili katika dakika za 71 na la pili katika dakika za nyongeza.
Kwa upande mwingine ushindi wa Simba umekuwa balaa kubwa kwa Ruvu Shooting inayochechemea mkiani katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 20 katika mechi 28 na sasa ni kama vile inasubiri siku tu za kutangazwa rasmi kushuka daraja na kuachana na Ligi Kuu NBC.
Soka Simba haijakata tamaa Ligi Kuu NBC
Simba haijakata tamaa Ligi Kuu NBC
Read also