London, England
Hatimaye kocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard amepata ushindi wa kwanza na timu hiyo baada ya mechi sita wakiilaza, Bournemouth mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.
Lampard, alikabidhiwa jukumu la kuinoa Chelsea mapema mwezi uliopita akichukua nafasi ya Graham Potter lakini amejikuta akiishuhudia timu hiyo ikichezea vichapo mfululizo zikiwamo mechi nne za EPL na mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Conor Gallagher dakika ya tisa, Benoit Badiashile dakika ya 82 na Joao Felix dakika ya 86 wakati bao pekee la Bournemouth waliokuwa wenyeji likifungwa na Matias Vina dakika ya 21.
Katika mechi ya jana, Lampard aliamua kubadili kikosi akiwaacha benchi Pierre-Emerick Aubameyang na Raheem Sterling ambao walikuwamo katika kikosi kilichochapwa mabao 3-1 n Arsenal.
Matokeo hayo yanaiweka pagumu Bournemouth inayoandamwa na janga la kushuka daraja zikiwa zimebakia mechi tatu kabla ya ligi kumalizika huku Chelsea nayo ikiwa kwenye nafasi ya 11.
Na ingawa Bournemouth ina pointi tisa zaidi ukilinganisha na timu tatu zinazopambana mkiani lakini lolote linaweza kutokea hasa kwa kuwa baadhi ya timu zimebakiwa na mechi nne.
Matokeo mechi za EPL za Jumamosi ni kama ifuatavyo…
Bournemouth 1-3 Chelsea
Man City 2-1 Leeds
Tottenham 1-0 Crystal Palace
Wolves 1-0 Aston Villa
Liverpool 1-0 Brentford
Kimataifa Lampard apata ushindi wa kwanza
Lampard apata ushindi wa kwanza
Read also