Na mwandishi wetu
Baada ya kipa chipukizi wa Simba, Ally Salim kuonesha kiwango kizuri kwenye mechi mbili za hivi karibuni, uongozi wa klabu hiyo unadaiwa kuwa mbioni kumpa mkataba mpya wa miaka mitatu.
Salim ambaye ni kipa namba tatu wa timu hiyo, alionesha kiwango kizuri kwenye mechi mbili za mwisho alizopewa nafasi dhidi ya Ihefu na Yanga ambazo zote walishinda kwa mabao 2-0.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ameeleza kuwa uwezo uliooneshwa na kipa huyo chipukizi umemvutia kocha wao Roberto Oliveira na kuagiza apewe mkataba mrefu.
“Robertinho ameuomba uongozi kumpa mkataba wa miaka mitatu kipa Ally Salim sababu amevutiwa sana na kiwango chake lakini amesema ndio mtu anayeweza kumpa ushindani mzuri Aishi Manula,” alisema Rweyemamu.
Meneja huyo ameeleza kuwa kocha Robertinho ameahidi kumuandalia utaratibu mzuri wa mazoezi pamoja na mechi za kucheza lengo likiwa ni kuhakikisha anapata uzoefu wa kutosha na anakuwa tegemeo kwenye kikosi cha Simba.
Alisema katika kipindi hiki ambacho Manula amepata majeraha yeye ndio kipa chaguo la kwanza na huenda akampa nafasi ya kucheza katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Soka Ali Salim kupewa miaka 3 Simba
Ali Salim kupewa miaka 3 Simba
Read also