London, England
Klabu ya Chelsea imemtimua kocha Graham Potter baada ya timu hiyo kufungwa na Aston Villa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England juzi Jumamosi.
Uamuzi wa kumtimua Potter umechukuliwa jana Jumapili ikiwa ni saa chache baada ya Leicester City nayo kumtimua kocha Brendan Rodgers baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Craystal Palace.
Chelsea imeshuka hadi nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nyuma kwa tofauti ya pointi 12 kutoka timu nne bora za EPL hali inayohatarisha ushiriki wa timu hyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Anguko la timu hiyo kwenye EPL limesababisha uamuzi huo mgumu kuchukuliwa hasa kwa kuwa takriban Pauni 550 milioni zimetumika kwenye usajili wa wachezaji wapya lakini matokeo yameendelea kuwa mabaya.
Wamiliki wa klabu hiyo wameeleza kusikitishwa na uamuzi wa kumtimua kocha huyo ambaye kwa mara ya kwanza alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo, Septemba mwaka jana akitokea Brighton.
Kwa mujibu wa Chelsea, Potter pamoja na kutimuliwa, amekubali kushirikiana na uongozi katika kipindi cha mpito ambapo Bruno Saltor aliyekuwa msaidizi wake akiwa Brighton sasa atabeba majukumu ya kocha mkuu.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa na matajiri wawili wa klabu hiyo, Todd Boehly na Behdad Eghbali ilimsifia Potter, “Tunamheshimu mno Graham kama kocha na binadamu, wakati wote alikuwa akiendesha mambo yake katika ubora na maadili na sote tunasikitishwa na hiki kilichotokea.”
Potter anakuwa kocha wa pili kutimuliwa Chelsea tangu kuanza msimu huu, kabla yake timu hiyo ilikuwa ikinolewa na Thomas Tuchel ambaye alitimuliwa lakini kwa sasa anainoa Bayern Munich ya Ujerumani.
Kimataifa Graham Potter atimuliwa Chelsea
Graham Potter atimuliwa Chelsea
Read also