Na mwandishi wetu
Kikosi cha timu ya Mbeya City, tayari kimewasili Singida kuikabili Singida Big Stars katika mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la FA (ASFC) utakaochezwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Liti.
Abdallah Mobiru ambaye ni Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema wamesafiri na kikosi chote lengo likiwa ni kushinda na kusonga mbele hatua inayofuata ya nusu fainali ya michuano hiyo.
“Tunakwenda kucheza na timu nzuri, ina wachezaji wazuri wenye uzoefu lakini hata sisi tumejipanga na tunataka kuingia kwenye rekodi za kubeba Kombe la FA msimu huu,” alisema Mobiru.
Kocha huyo ameeleza kuwa kusimama kwa ligi kumemsaidia kukiimarisha kikosi chake na kuwasoma vizuri wapinzani wao Singida, hiyo mchezo wao wa keshokutwa utakuwa mzuri sababu hawatocheza kwa kujihami sababu wanahitaji ushindi.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Mbeya City kufika hatua hiyo kwenye michuano hiyo ya Kombe la FA ambayo huu ni msimu wa nane tangu kuanzishwa kwake.
Soka Mbeya City wapo Singida
Mbeya City wapo Singida
Read also