Dortmund, Ujerumani
Klabu ya Real Madrid imeanza mazungumzo na kiungo wa Borrusia Dortmund ya Ujerumani na timu ya Taifa ya England, Jude Bellingham yenye lengo la kumsajili mchezaji huyo.
Wawakilishi wa klabu hiyo ya Hispania inadaiwa wamefika Ujerumani hivi karibuni kwa ajili ya kukutana na Bellingham na familia yake nia ni kuhakikisha anajiunga na vigogo hao wa Hispania.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, katika mpango wa kumsajili kiungo huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 19, Real Madrid imetenga Pauni 88 milioni na fedha za ziada Pauni 35 milioni.
Habari za awali zinadai kuwa, Bellingham yumo katika hesabu za Real Madrid lengo likiwa kukiimarisha kikosi cha timu hiyo kwa kusajili wachezaji bora wa bei mbaya na wenye umri mdogo.
Katika mpango huo pia yumo mshambuliaji nyota wa Man City, Erling Haaland ambaye habari zisizo rasmi zinadai kwamba kwenye mkataba wake na Man City kuna kipengele kinachomruhusu kuihama timu hiyo.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amewahi kukana kuwapo kipengele cha aina hiyo lakini inaaminika kwamba dhamira wa Real Madrid kumchukua Haaland imeendelea kuwa pale pale.
Kama ilivyo kwa Bellingham mwenye miaka 19 na tayari amethibitisha ubora wake akiwa na England pamoja na Dortmund, ni hivyo hivyo kwa Haaland naye ndio kwanza ana miaka 22 na tayari dunia nzima inatambua uwezo alionao katika kuzifumania nyavu.
Kimataifa Madrid yamfuata Bellingham Ujerumani
Madrid yamfuata Bellingham Ujerumani
Read also