Madrid, Hispania
Kamati inayoendesha kampeni kupinga vurugu nchini Hispania imependekeza shabiki wa soka mbaguzi wa rangi apewe adhabu ya kutoruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya michezo kwa mwaka mmoja.
Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatuhumiwa kumtamkia maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius Junior
Kauli ya kamati hiyo imekuja wakati ambao mashabiki wanasubiri kuona adhabu atakayopewa shabiki huyo ambaye anatuhumiwa kumtamkia Vinicius maneno hayo Februari 5 mwaka huu.
Siku ya tukio hilo, shabiki huyo anayeaminika kuwa ni wa klabu ya Real Mallorca alikuwa uwanjani wakati timu hizo zikichuana katika mechi ya Ligi Kuu Hispania maarufu La Liga.
Shabiki huyo anayedaiwa kuwa na tiketi ya msimu aligunduliwa na maofisa usalam huku ikidaiwa ndiye aliyemtamkia maneno ya kibaguzi mchezaji wa Villarreal, Samu Chukwueze ambaye kama Vinicius wote wana asili ya Afrika.
Vinicius pia alikumbana na adha ya kauli za kibaguzi mara baada ya mechi na Mallorca alipokuwa amesimama kwa ajili ya kupiga picha na mashabiki pamoja na kusaini vitabu vya kumbukumbu.
Mchezaji huyo ambaye pia amejikuta akisakamwa na mashabiki kwa kutamkiwa maneno ya kibaguzi tangu alipoanza kucheza soka Hispania takriban miaka mitano iliyopita.
Wasimamizi wa La Liga wamewahi kufikisha matukio ya kibaguzi dhidi ya Vinicius katika vyombo vya sheria lakini baadhi ya matukio hayo yamefutwa na waendesha mashitaka.
Kimataifa Wataka aliyembagua Vinicius afungiwe mwaka
Wataka aliyembagua Vinicius afungiwe mwaka
Read also