Na mwandishi wetu
Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) kinatarajia kutoa mafunzo ya ukocha kuanzia ngazi ya awali, daraja la kwanza na la pili itakayofanyika kwa siku 10 Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi alisema mafunzo hayo yatafanyika mwishoni mwa mwezi ujao na kuhimiza wadau mbalimbali wanaopenda mchezo huo kujitokeza kujisajili.
Alisema ada ya kujisajili ni Sh 5,000 na gharama nyingine za uendeshaji wa mafunzo hayo ni Sh 100,000 na kwamba mafunzo yatakayotolewa ni muhimu kwa wengi kujitokeza ili waandaliwe namna ya kuwaandaa wachezaji bora wa mchezo huo katika ngazi zote.
“Tulikuwa tufanye mafunzo haya Morogoro lakini tukaona ushiriki mkubwa wa watu unatoka Dar es Salaam tukahamisha, malengo yetu tumedhamiria kuzalisha walimu wengi kwa ajili ya kusaidia kwenda kuibua vipaji,” alisema.
Mkisi alisema mafunzo yatafundishwa na wakufunzi waliobobea katika mchezo huo na tayari wamewapata wanachosubiri ni ushiriki wa watu uongezeke hadi kufika mwishoni mwa mwezi Machi, mwaka huu kuwe na idadi kubwa ya watu.
Sports Mix Makocha netiboli kufanyiwa semina siku 10
Makocha netiboli kufanyiwa semina siku 10
Related posts
Read also