Barcelona, Hispania
Saa kadhaa kabla ya mechi kati ya Barca na Man United, kocha wa Barca, Xavi Hernandez alimpamba Marcus Rashford akisema ni mshambuliaji hatari, Rashford kathihitisha hilo baada ya kufunga bao timu hizo zilipoumana na kutoka sare ya mabao 2-2.
Barca na Man United ziliumana jana Alhamisi usiku katika mechi ya kwanza ya Europa Ligi iliyopigwa kwenye dimba la Nou Camp na kumshuhudia Rashford akifunga bao moja na kutoa mchango mkubwa kwa bao la pili.
Rashford kwa sasa yuko katika msimu bora akiwa tayari amezifumania nyavu mara 22 katika mashindano yote msimu huu huku kukiwa na kila dalili kwamba ataendelea kuibeba timu yake.
“Marcus Rashford yuko moto, yuko katika kiwango tofauti, kiwango ambacho hakuwahi kuwa hapo kabla, ameweza kuwa katika kiwango kile kile hadi sasa, anajiamini, si wa kumdharau,” alisema beki wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand.
Katika mechi 16 zilizopita, mshambuliaji huyo wa England ambaye ana miaka 25 amefunga mabao 14, rekodi ambayo inadhihirisha ubora wa mshambuliaji mwenye uwezo wa kuzifumania nyavu.
Wenyeji Barca ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Alonso dakika ya 50, Rashford akasawazisha dakika mbili baadaye na Kounde akajifunga dakika ya 56 kabla Raphinha hajaisawazishia Barca dakiika ya 76.
Matokeo ya mechi za Europa Ligi ni kama ifuatavyo…
Barca 2-2 Man Utd
Ajax 0-0 Union Berlin
RB Salzburg 1-0 Roma
Shakhtar Donetsk 2-1 Rennes
B Leverkusen 2-3 Monaco
Juventus 1-1 Nantes
Sevilla 3-0 PSV Eindhoven
Sporting 1-1 FC Midtjylland