London, England
Chama cha Soka England (FA), kimeanzisha uchunguzi baada ya mchezaji wa Man City, Kevin de Bruyne kurushiwa vitu uwanjani katika mechi na Arsenal ambayo City ilishinda kwa mabao 3-1.
De Bruyne alikumbana na kadhia hiyo wakati akitoka uwanjani na inaaminika mwamuzi wa mchezo huo uliochezwa juzi Jumatano, Anthony Taylor amelitaja tukio hilo katika ripoti yake.
Arsenal wanachunguza tukio hilo kupitia picha za CCTV na kuahidi kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika. “Hili jambo halikubaliki na halivumiliki,” alisema msemaji wa Arsenal.
De Bruyne katika mechi hiyo alifunga goli na kutoa pasi iliyozaa goli na kuipa City matokeo ambayo yameifanya iiengue Arsenal kileleni ingawa timu hizo zinalingana kwa pointi zote zikiwa na pointi 51 City ikineemeka na idadi ya mabao ya kufunga na City imecheza mechi moja kuizidi Arsenal.
Katika kinachoonekana kudhihaki tukio hilo, De Bruyne alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii ikiwa na maneno, ‘asanteni’ na nyingine yenye ujumbe unaozungumzia unywaji wa bia.
Kimataifa FA wachunguza kadhia ya De Bruyne
FA wachunguza kadhia ya De Bruyne
Read also