Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Azam, Kipre Junior ameeleza furaha aliyonayo baada ya juzi kufanikiwa kuifungia timu hiyo bao lake la kwanza huku akiahidi kuwa atapambana kuhakikisha anafunga zaidi.
Kipre raia wa Ivory Coast aliyetua Azam msimu huu amefanikiwa kutoa pasi za mabao tano lakini hakuwahi kufunga kabla ya kufanya hivyo juzi walipoitungua Tanzania Prisons mabao 3-0.
“Nina furaha sana kufunga bao na kuisaidia timu yangu, ni muhimu sana kuisaidia timu kupata ushindi na leo nimefunga goli langu la kwanza katika ligi nimefurahi sana na sasa imeleta furaha kwa timu yote,” alisema Kipre.
Pamoja na hayo, amekiri kuwepo kwa maoni ya kumkosoa kutokana na kutowahi kuifungia Azam bao kwenye ligi tangu atue akitokea Sol FC ya nchini kwao lakini huwa hasikilizi maoni hayo zaidi ya kuendelea kupambana kutimiza ndoto zake.
“Nafahamu maneno yanakuwepo lakini huwa sisikilizi maoni mabaya ya watu wanayosema kwenye mitandao kuhusu mimi katika kufunga mabao zaidi nazingatia kazi yangu nikitazamia kuhakikisha naipatia ushindi zaidi timu yangu kwa kufunga,” alisema Kipre.
Soka Kipre afurahia bao la kwanza Azam
Kipre afurahia bao la kwanza Azam
Related posts
Read also