Manchester, England
Baada ya Man City kufungwa mabao 2-1 na Man United, kocha wa Man City, Pep Guardiola amekerwa na bao la Bruno Fernandez akidai mechi hiyo isingechezwa Old Trafford bao hilo lingekataliwa.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL) iliyochezwa Jumamosi hii, Fernandez alifunga bao ambalo awali lilikataliwa kwa kuwa Marcus Rashford alikuwa katika eneo la kuotea lakini lilikubaliwa kwa kuwa mchezaji huyo aliuacha mpira uliomkuta Fernandes ambaye hakuwa katika eneo la kuotea.
Wachezaji wa Man City walilalamikia sana bao hilo wakidai kwamba Rashford alihusika mchezoni na Pep akadai baadaye kwamba Man United walipewa bao hilo kutokana na nguvu ya mashabiki waliokuwa uwanja wa nyumbani.
“Rashford alikuwa eneo la kuotea, Bruno hakuwa eneo hilo, suala hapa ni kuhusika, mchezaji mmoja anapopiga mpira akiwa eneo la 18 na mwingine yuko mbele ya kipa lakini haugusi mpira, wakati wote hilo haliruhusiwi,” alisema.
“Mazingira yote na tukio ni ya mwamuzi na VAR, mabeki wetu walijipanga (kwa ajili ya Rashford) kama tungejua kuwa ni Fernandez tusingejipanga, tunafuata tukio na baada ya tukio ni kila anayehusika,”alisema Pep.
“Haya ni maamuzi kwenye uwanja huu kwa waamuzi na kwa VAR, hapa hayaingiliwi kwenye uwanja huu, sisi kina nani hadi tuingilie? Je tutakwenda kulalamika? Hapana, kuna wakati inatokea hata upande wetu,” aliongeza.
“Huu ni uamuzi ambao hawaamini Rashford alihusika katika uwanja huu, hapa ni Old Trafford, ni lazima tucheze vizuri zaidi, ni kama Anfield, ni lazima tuwe bora zaidi,” alisisitiza.
Katika mechi hiyo, City ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Grealish katika dakika ya 60 kabla ya United kusawazisha dakika ya 78 kwa bao la Fernandez wakati la pili lilifungwa na Rashford.
Katika mechi nyingine za EPL za Jumamosi matokeo ni kama ifuatavyo…
Man Utd 2-1 Man City
Brighton 3-0 Liverpool
Everton 1-2 Southampton
Nottm Forest 2-0 Leicester
Wolves 1-0 West Ham
Brentford 2-0 Bournemouth
Kimataifa Bao la Fernandez lamkera Pep
Bao la Fernandez lamkera Pep
Read also