Na mwandishi wetu
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Coastal Union, Yusuf Chipo ameitakia kila la heri timu hiyo ikiwa ni muda mfupi tangu afutwe kazi huku akieleza hana kinyongo kwa kuondolewa katika timu hiyo.
Coastal imetangaza leo kuachana na kocha huyo raia wa Kenya kutokana na matokeo yasiyoridhisha huku mikoba yake akipewa kocha msaidizi, Joseph Lazaro.
Chipo alisema anaamini viongozi wa Coastal waliona jahazi linamshinda ndiyo maana wamefikia maamuzi hayo ambayo ni ya kawaida kwa taaluma yake kwamba makocha wanaajiriwa kwa ajili ya kufukuzwa.
“Tumeachana na si kwamba nimeachia jahazi isipokuwa nimeachishwa jahazi, nafikiri waliona linanielemea ndiyo maana nimeyapokea maamuzi hayo, niwatakie kila la heri pia maana ndiyo taaluma yetu kwamba hata ukiingia uchukue makombe 10 ikifika muda wako utaondoka tu,” alisema Chipo.
Chipo ambaye alirejea mara ya pili kuinoa Coastal msimu huu akichukua mikoba ya Juma Mgunda aliyetimkia Simba, ameiacha timu hiyo katika nafasi ya 13 baada ya kuiongoza kwenye mechi 13 ambapo alishinda tatu, sare mbili na kufungwa michezo minane.
Soka Chippo aaga Coastal, hana kinyongo
Chippo aaga Coastal, hana kinyongo
Read also