Na mwandishi wetu
Kama Yanga ilianza kibabe mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC, Simba imeuanza mzunguko huo kwa kishindo leo Jumapili kwa kuilaza Geita Gold mabao 5-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Simba inakuwa imeijibu Yanga ambayo jana Jumamosi iliuanza mzunguko wa pili wa ligi kwa kuichapa Polisi Tanzania mabao 3-0 na leo Simba imejibu mapigo kwa kishindo kwa kupata ushindi mnono ambao umewafanya kuimarisha rekodi yao ya mabao ya kufunga wakiwa wamefikisha jumla ya mabao 36 na point zao 37.
Yanga ndiyo inayoshika usukani ikiwa na pointi 41 wakati Simba inashika nafasi ya pili na Azam ni ya tatu ikiwa na pointi 36, timu zote hizo hadi sasa zimecheza mechi 16.
Simba leo ilianza kuinyanyasa Geita katika dakika ya 12 kwa bao lililofungwa na nahodha John Bocco kabla Clatous Chama hajaandika bao la pili katika dakika ya 40 na kuzifanya timu ziende mapumziko Simba ikiwa na mabao mawili mkononi.
Dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili, Pape Sakho aliiandikia Simba bao la tatu kabla ya kuongeza bao la nne katika dakika ya 75 wakati bao la mwisho la Simba lilifungwa na Dennis Kibu dakika moja kabla ya mpira kumalizika.
Soka Simba yaipiga Geita Gold 5-0
Simba yaipiga Geita Gold 5-0
Read also