Manchester, England
Manchester United imekubali kulipa Pauni 80.75 milioni ili kumsajili winga wa Ajax, Antony ambaye sasa anakuwa mmoja wa wachezaji waliosajiliwa kwa bei mbaya.
Baada ya Paul Pogba ambaye alisajiliwa kwa ada ya Pauni 89 milioni na ndiye anayeshikilia rekodi ya mchezaji aliyenunuliwa na Man United kwa bei mbaya, Antony naye sasa anaingia katika orodha hiyo ya wachezaji wa bei mbaya.
Antony anabebwa na mafanikio ambayo ameyapata akiwa Ajax kwa kufunga mabao 25 na asisti 82 tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2020 akitokea Sao Pulo ya Brazil lakini kubwa zaidi ni kwamba kocha wa sasa wa Man Utd, Erik ten Hag anamjua vizuri mchezaji huyo uwezo wake kwani amewahi kuwa naye wakati huo akiwa kocha Ajax.
Akiwa ndio kwanza ana miaka 22, Antony alianza kuichezea timu ya Taifa ya Brazil, Oktoba 2021 na tayari ana mabao mawili katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo wakati akiwa na Ajax hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao saba katika mechi 11 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Haijaweza kueleweka mara moja iwapo Antony anayetumia vizuri zaidi mguu wa kushoto kama atavaa jezi ya Man Utd, Alhamisi hii siku ambayo timu hiyo itaumana na Leicester City katika mechi ya Ligi Kuu England kwa kuwa suala hilo pia linahusisha upatikanaji wa kibali cha kufanyia kazi Uingereza.
Anatony anakuwa mchezaji wa tano wa Man Utd kusajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya mchezaji mwenzake wa Ajax, beki Lisandro Martinez, kiungo Casemiro kutoka Real Madrid, beki Tyrell Malacia kutoka Feyernoord na kiungo mchezeshaji Christian Eriksen.
Usajili wa Antony pia unazidisha uvumi kuhusu majaliwa ya Cristiano Ronaldo katika klabu hiyo hasa baada ya kuwapo habari za muda mrefu kwamba mchezaji huyo alikuwa akitaka kuihama timu hiyo.
Kimataifa Antony atua Man Utd kwa pesa ndefu
Antony atua Man Utd kwa pesa ndefu
Read also